Gamondi asisitiza, wataiheshimu Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2024
Gamondi asisitiza, wataiheshimu Simba

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anakiandaa kikosi chake pasipo na presha yoyote akiamini maandalizi bora ndio yatawapa nafasi ya kushinda mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi April 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kocha huyo raia wa Argentina amesisitiza ni lazima wafanye maandalizi makini kwani anafahamu mchezo huo wa duru ya pili utakuwa mgumu pengine kuliko mchezo wa kwanza ambao kikosi chake kiliibuka na ushindi wa mabao 5-1

"Sisi tunajiandaa pasipo kuwa na presha yoyote, hii ni mechi kama zilivyo mechi nyingine za ligi kuu, ushindi ni alama tatu"

"Nafahamu kile ambacho mashabiki wetu wanazungumza kuelekea mchezo huu lakini sisi tunajiandaa kama tulivyofanya kwenye mechi zilizopita, tumeweka weledi mbele"

"Hatujacheza mechi rahisi msimu huu, tumeshinda mechi hizi zote kwa kutanguliza weledi kwa kuwaheshimu kwanza wapinzani wetu bila kujali changamoto zao"

"Tunauhitaji ushindi huu kama ambavyo tumekuwa tukihitaji kushinda mechi zilizopita, tutakwenda kucheza mechi hii bila presha kwa kutumia falsafa yetu kuweza kushinda mechi hii na haitakuwa rahisi kabisa," alisema

Ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa duru ya kwanza na ubora wa kikosi, umewapa mashabiki Yanga matumaini ya kuibuka na ushindi siku ya Jumamosi

Hata hivyo mara nyingi derby wakati mwingine huamuliwa na dakika 90 pasipo kujali matokeo ya nyuma au mwenendo wa timu katika wakati husika

Hii ndio sababu ya Yanga kuchukua tahadhari kubwa kuelekea mchezo huo. Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kuwa maandalizi wanayofanya kuelekea mchezo huo ni zaidi ya maandalizi waliyofanya wakati wakijiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’