Haikuwa mechi rahisi - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2024
Haikuwa mechi rahisi - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema licha ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, amekiri kuwa haikuwa rahisi huku akiwamwagia sifa mastaa wake kwa kufanya kazi kwa usahihi.

Gamondi ameyasema hayo muda mchache baada ya kukamilika kwa mchezo wa Kariakoo Dabi ambapo Yanga imefisha pointi 58 na kuendelea kujikita kileleni wakiwaacha Azam FC ambao wapo nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi saba. Simba yenye pointi 46 katika nafasi ya tatu, imeachwa pointi 12.

Mbali ya kuwapongeza wachezaji wake kwa kufanya vizuri, lakini pia wamepiga hatua kubwa katika harakati za kutetea taji lao la Ligi Kuu Bara wanalolishikilia.

"Kupata matokeo mbele ya Simba sio rahisi, timu inatakiwa kupambana kutokana na mpinzani kuwa imara, na hicho kimefanywa na wachezaji wangu ambao walifuata maelekezo niliyowapa," amesema na kuongeza;

"Siwezi kusema nani alikuwa bora kati ya wachezaji wangu, wote wameonesha ubora ambao sio rahisi kuonekana kama wote wasingekuwa na uwezo.

"Kiufundi wote wamenivutia kwani kila mchezaji ametekeleza majukumu yake na kinachofuata sasa ni kusonga mbele. Mchezo huu umemalizika, sasa uelekeo ni katika mechi zilizobaki ili kujihakikishia ubingwa msimu huu"

Yanga imebakiwa na mechi nane, inatakiwa kupata ushindi katika mechi sita ili kufikisha pointi 76 ambazo hazifikiwa na Azam wala Simba, hivyo itatangaza ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’