Ligi Kuu ya NBC iko katika hatua za lala salama mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga leo wakitarajiwa kushuka dimba la Meja Jen. Isamuhyo kuwakabili maafande wa JKT Tanzania
Ni mechi ya mzunguuko wa 23 inayotarajiwa kupigwa majira ya saa 10 jioni
Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zinafanya mazingira ya mchezo huo kuwa magumu lakini Wananchi hawatakuwa na namna zaidi ya kupambana ili kuondoka na alama zote tatu
Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani zao Simba mwishoni mwa wiki, Yanga ilirejea mazoezini jana na kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo, ni wachezaji wawili tu Joyce Lomalisa na Pacome Zouzoua ambao hawatakuwa sehemu ya mchezo
Yanga inasaka ubingwa wa tatu mfululizo ligi kuu ya NBC na kama wananchi wataibuka na ushindi, watasogea karibu zaidi kwani watahitaji kushinda mechi nyingine nne kuwa mabingwa