Yanga kuitumia Singida United kujiandaa kuikabili Dicha ugenini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
10 Apr 2018
Yanga kuitumia Singida United kujiandaa kuikabili Dicha ugenini
Kocha Mkuuwa Yanga, George Lwandamina amesema kwamba atautumia mchezo dhidi ya Singida United kesho kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wa marudiano na Wolaita Ditcha wiki ijayo nchini Ethiopia.

Yanga SC inatarajiwa kuwakaribisha Singida United kesho Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikihitaji ushindi ili kuweka hai matumaini ya kutetea taji.

Yanga itaingia kwenye mchezo wa kesho ikitoka kushinda 2-0 dhidi ya Wolaita Ditcha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi Uwanja wa Taifa.

Timu hizo zitarudiana Jumatano ya wiki ijayo, Aprili 18 Uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia

Kwenye mahojiano na mtandao wa Bin Zubeiry, Lwandamina amesema kwamba mchezo dhidi ya Singida utakuwa mgumu, lakini watajitahidi washinde ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.

“Singida ni timu nzuri na tumetoka kucheza nayo wiki iliyopita tu pale Singida kila mtu ameona matokeo, maana yake mechi ya Jumatano itakuwa ngumu, vizuri hata wachezaji wangu wanalijua hilo. Tunajipanga.

"Kwetu tutautumia mchezo huu pia kama sehemu ya maandalizi yetu ya mechi ya marudiano na Ditcha,”amesema Lwandamina.

Mapema mwezi huu, Aprili 1 Singida United waliitupa nje Yanga SC kwenye Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup kwa ushindi wa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Hivyo kesho Yanga pamoja na kuhitaji pointi kwa ajili ya kuongeza kasi ya kuwafukuzia mahasimu wao, Simba SC pale kileleni, lakini pia itataka kulipa kisasi kwa timu ya kocha wao wa zamani, Mholanzi, Hans van der Pluijm.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →