Gamondi apania ushindi dhidi ya Coastal Union

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2024
Gamondi apania ushindi dhidi ya Coastal Union

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema baada ya kupata sare mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, vijana wake wako tayari na wamepania kupata ushindi dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex

Gamondi amesema anatambua ubora wa Coastal Union katika kuzuia lakini wamejipanga na matokeo pekee wanayohitaji katika mchezo huo ni ushindi

"Tumetoka kucheza mchezo kwenye mazingira magumu na tuna njaa ya kupata alama tatu. Hautakuwa mchezo rahisi kwasababu Coastal ni wazuri kwenye kuzuia mashambulizi, lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho"

"Mechi zinapokuwa karibu sana muda wa maandalizi unakuwa mdogo, jana tumefanya mazoezi ya kurejesha miili sawa kwa Wachezaji na leo tutapata muda kidogo wa kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa kesho na hapo ndipo nitajua Wachezaji wa kuwatumia"

"Mchezo wa kesho unahitaji sana ubora wa Wachezaji na angalau tunaenda kucheza kwenye Uwanja wenye mazingira mazuri, muhimu zaidi kesho ni kuweka mpira wavuni na kuibuka na ushindi," alisema Miguel Gamondi

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinda lango Aboutwalib Mshery amesema baada ya kukosa ushindi katika mchezo uliopita, wataingia kuikabili Coastal Union kusaka ushindi

"Tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunapata alama 3 kesho, Coastal wako kwenye ubora mzuri sasahivi na sisi tunajua hatuwezi kuwa Mabingwa bila kupambana na timu ngumu," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’