Jana Mamelodi Sundowns waliaga michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kipigi cha bao 1-0 kutoka kwa Esperance katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali
Esperance wametinga fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0 baada ya pia kushinda bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Kipigo hicho ni sehemu ya haki kwa Yanga kwani Sundowns hawakustahili kuingia nusu fainali, pengine nafasi hiyo ilistahili kuwa ya Yanga
Bao la dakika ya 57 lililofungwa Stephane Aziz Ki lilikataliwa hadharani ukiwa ni mkakati wa kuhakikisha Sundowns inayomilikiwa na Rais wa CAF Patrece Motsepe inasonga mbele
Jana wamepata haki yao katika uwanja uleule ambapo wakati huu bao la Esperance halikuhitaji VAR
Esperance watachuana na Al Ahly katika mchezo wa fainali baada ya Ahly nao kushinda mabao 3-0 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa nusu fainali