Bao la Joseph Guede limeihakikishia Yanga alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Yanga iliingia katika mchezo huo kwa ari kubwa ya kusaka matokeo pengine Wananchi wangeweza kumaliza mechi hiyo katika kipindi cha kwanza kama Guede angekuwa makini kutumia nafasi adimu alizopata
Hata hivyo Guede alisahihisha makosa yake kwa kuifungia Yanga bao pekee dakika ya 76 kwa shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari
Hilo lilikuwa bao lake la nne ndani ya ligi kuu msimu huu likiwa bao la saba katika mashindano yote
Alama 62 kwa Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi, dalili zinaonekana kuelekea ubingwa wa 30
ADVERTISE HERE