Kiungo mshamnbuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amefunguka kuwa yuko tayari kurejea uwanjani baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani wiki tano
Kukosekana kwake kwa muda mrefu kumeibua maswali mengi na ikapelekea baadhi ya wale wasioitakia mema Yanga kuibua za upotoshaji wakidai mchezaji huyo amefungiwa na wengine wakienda mbali zaidi wakitaka TFF waipokea Yanga alama wakidai mchezaji huyo alitumika huku usajili wake ukiwa na dosari
"Sasa hivi niko sawa, namshukuru daktari wa mazoezi ya viungo (Taibi) amehakikisha naimarika na kuwa tayari kurejea uwanjani"
"Najiona nimepona kwa asilimia 100 na niko tayari kurejea tena uwanjani kuitumikia Yanga," Pacome aliiambia Yanga TV
Kiungo huyo aliyeifungia Yanga mabao matatu katika ligi ya mabingwa huku akiwa na mabao saba kwenye ligi kuu ya NBC, amewashukuru mashabiki ambao wamekuwa nae kwa sala na maombi katika kipindi chote alichokuwa majeruhi
"Nawashukuru mashabiki wa Yanga, kila wanaponiona wananiita na kuniombea niweze kupona. Nimepokea sms nyingi kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wananiombea ili niweze kurejea uwanjani haraka"
"Ninafarijika na kupata moyo kuona mchango wangu unathaminiwa na kila mmoja hapa"
Pacome amesema anaamini ataanza kupata muda wa kucheza katika mechi zinazofuata na ataendelea kuimarika kadiri atakapokuwa akicheza mechi za ushindani
Amesema jambo pekee ambalo anafikiria sasa ni kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambapo kama timu watahakikisha lengo hilo linafanikiwa
Pengine Wananchi wwatarajie kumuona katika mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Tabora United utakaopigwa Jumatano May 1 katika uwanja wa Azam Complex