Yanga inataka nne bora Afrika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2024
Yanga inataka nne bora Afrika

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema malengo ya mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu ujao ni kuona wanakuwa miongoni mwa timu nne bora barani Afrika na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia la klabu

Akizungumza katika mahojiano na Bongo Fm mapema leo, Hersi amesema kwa sasa Yanga ndio klabu bora hapa Tanzania na hilo wameridhihirisha msimu huu

"Kwa sasa hakuna Klabu Tanzania inayoweza kuisogelea Yanga kwenye ubora. Ndio maana timu nyingi zikicheza na sisi zinakuja na mfumo wa kuzuia zaidi ikimaanisha wanaiheshimu Klabu yetu"

"Malengo yangu makubwa ni kuhakikisha Klabu yetu inakuwa moja ya Klabu bora Afrika. Na matamanio yangu ni kuona mwakani kwenye mashindano ya Kimataifa tufike katika orodha ya timu nne bora AFRIKA, ili tuweze kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu. Mwaka jana tumefika fainali na tumepata alama nyingi ambazo zitatuongezea nguvu ya kushiriki Kombe hilo," alisema Hersi

Hersi amesema wataendelea kufanya maboresho ya kikosi kwa kuzingatia mahitaji na jambo muhimu ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wachezaji bora

"Usajili ni sanaa, ni lazima ujue kwanini unafanya huo usajili. Kwa kifupi huwezi kubaki na wachezaji wako wazuri kwa muda wote, hivyo inabidi utengeneze mazingira mazuri ya kuvutia Wachezaji wengine wazuri"

"Hivyo nilichukua maamuzi ya kusimamia mchakato wa usajili. Unapokuwa Kiongozi lazima uwe na maono makubwa sana na uelewa mkubwa wa mpira"

"Unapaswa kujua mchezaji yupo kwenye kilele cha ubora wake, anapata wakati mgumu kuzuoea mazingira, amechoka nk. Usipokuwa na uelewa wa mpira basi utajikuta unasajili hovyo au unatimua wachezaji kwa hisia," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’