Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amewashauri wale wanaoeneza propaganda kuhusu wachezaji wa Yanga, watumie nguvu hizo kuzishauri timu zao zijenge timu ili kuleta upinzani wa kweli kwa Yanga
Simon ametoa kauli hiyo baada ya kuenezwa kwa propagana kumuhusu kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua
"Ndugu zangu watani na wale waeneza propaganda, tumieni nguvu hizo kuwashauri viongozi wa timu mnazoshabikia wajenge timu zenu ili mtupe changamoto ligi yetu iendelee kuwa bora"
"Mchezaji mpaka anacheza CAF Champions League mnadhani anajipeleka tu uwanjani!? Hamjui CAF wanatoa leseni!?"
"Tuwekeze kwenye mijadala ya kujenga na kuzisaidia timu zetu, propaganda mfu hazina ustawi wa soka letu"
"Hivi ndo mnataka ubingwa wa mezani sio!? Haya tukishalichukua Kombe tutawaletea mlichukue," aliandika Simon katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
'Wapika propaganda' hao walihusisha taarifa ya Yanga kufungiwa kusajili na FIFA na kutoonekana uwanjani kwa Pacome licha ya kufahamu kiungo huyo alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc March 17
Kifungo cha Yanga kutoka FIFA kilihusiana na kutokamilika kwa taarifa za malipo ya mchezaji (ambaye hakutajwa). FIFA iliizuia Yanga kusajili hadi pale itakaposahihisha mapungufu hayo
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imethibitisha kuwa tayari mapungufu hayo yamerekebishwa na kifungo hicho kimeondolewa