Yanga imezuiwa tena kusajili kutokana na madai ya mshambuliaji Lazarus Kambole
Kambole alishinda kesi ya madai dhidi ya Yanga na FIFA kuwataka mabingwa hao wa Tanzania Bara wamalizane nae katika kipindi cha siku 45
Hata hivyo kifungo hicho kitaondolewa pale Yanga itakapokamilisha malipo ya mchezaji huyo ambaye usajili wake umeitia tu hasara Yanga kwani hakutumika katika mechi za mashindanoย
Msimu uliopita Yanga ilimtoa kwa mkopo Zesco United ambapo alihitimisha mwaka wa pili wa mkataba wake
Yanga ilimsajili Kambole kutoka klabu ya Kaizer Chiefs 2022/23. Ni katika msimu huo pia Yanga ilimsajili Gael Bigirimana ambaye pia alishinda kesi ya madai dhidi ya Yanga
Yanga ililazimika kuachana na wachezaji hao baada ya kutokidhi mahitaji ya benchi la ufundi wakati huo Yanga ikinolewa na Nasreddine Nabi
Nafasi ya Kambole ilichukuliwa na Tuisila Kisinda ambaye amerejea RS Berkane baada ya muda wake wa mkopo na Yanga kumalizika
Nafasi ya Bigirimana ilichukuliwa na Kennedy Musonda