Mshambuliaji Joseph Guede anachuana na mlinda lango Djigui Diarra na kiungo Jonas Mkude katika tuzo ya mchezaji bora wa Yanga kwa mwezi April 2024
Mshindi wa tuzo hiyo inayodhaminiwa na NIC anaondoka na kitita cha Tsh Milioni 4 ambapo kura zinapigwa kupitia App ya Yanga
Guede amekuwa na kiwango bora mwezi April akifunga mabao manne huku Mkude akin'gara zaidi katika mechi ya robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns


Kwa upande wa Diarra mechi sita alizokaa langoni mwezi April aliruhusu bao moja tu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 2-1
Je tuzo ni ya Guede, Mkude au Diarra?
ADVERTISE HERE