Licha ya kutopata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari jana amedhihirisha bado yuko mara na anaweza kumpa changamoto Yao Kouassi
Jana Kibwana alicheza kwa dakika zote 90 katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Bank dhidi ya Tabora United Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0
Kibwana alitengeneza bao la kwanza lililofungwa na Stephane Aziz Ki huku akionyesha kiwango bora kwa dakika zote 90 za mchezo


Kibwana bado yupo kwenye mipango ya kocha Miguel Gamondi akiwa miongoni mwa wachezaji watakaosini mikataba mipya
Mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni wa msimu huu
ADVERTISE HERE