Uongozi wa Yanga tayari umeanza mazungumzo na nahodha wake Bakari Nondo Mwamyeto ili kumuongezea mkataba
Mwamnyeto mmoja wa walinzi ghali waliowahi kusajiliwa na Yanga, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu
Meneja wa Mwamnyeto, Carlos Sylivester amethibitisha mazungumzo ya kuhuisha mkataba wa mteja wake yameanza na Yanga ina nafasiku kubwa ya kumbakisha licha ya kukiri zipo ofa kutoka timu nyingine pia
"Siwezi kusema ofa nyingine zimetoka wapi ila zipo hadi za nje lakini klabu yake (Yanga) imeonyesha nia ya kumbakisha na tayari tumeshaanza mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya na yanaendelea vizuri," alisema Carlos
Mwamnyeto amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa misimu mitatu sasa akijiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara akitokea klabu ya Coastal Union
Yanga pia inatajwa kuwa kwenye mchakato wa kuwaongeza mikataba nyota wengine wa ndani, Kibwana Shomari na Nickson Kibabage