Kama mambo yatakwenda vizuri, mshambuliaji Clement Mzize anaweza kwenda barani Ulaya kucheza soka la kulipwa
Yanga imepokea ofa kutoka nchi za Urusi na Israel kwa ajili ya mchezaji huyo kwenda kucheza soka la kulipwa
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha ujio wa ofa hizo ambapo amebainisha kuwa mazungumzo yanaendelea
Kamwe amegoma kutaja klabu zinazomtaka mchezaji huyo kwa kuwa bado mazungumzo yanaendelea lakini amedokeza ni timu zinazoshiriki ligi kuu
"Ni kweli tumepokea ofa kwa ajili ya mchezaji wetu Mzize (Clement) mazungumzo bado yanaendelea. Huu sio wakati wa kuweka kila kitu wazi kwa kuwa mazungumzo bado hayajakamilika lakini ofa hizo zimetoka nchi za Urusi na Israel," alisema
Alikuwa ni kocha Nasreddine Nabi aliyempandisha Mzize kikosi cha kwanza kutoka timu ya U20 na hata kocha wa sasa wa Yanga Miguel Gamondi amemuamini na anamtumia sawa na washambuliaji wengine Joseph Guede na Kennedy Musonda
Awali kulikuwa na tetesi Azam Fc walikuwa wakimnyemelea kabla ya Yanga kumuongeza mkataba wiki kadhaa zilizopita