Guede apania rekodi ya mabao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2024
Guede apania rekodi ya mabao

Baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa robo fainali ya mashindano ya Kombe la FA, mshambuliaji wa Yanga, Joseph Guede, amejiwekea malengo ya kufunga angalau mabao 17 katika mashindano yote

Guede ambaye alianza kwa kusuasua, kwa sasa amekuwa 'moto', akifunga mabao muhimu kwa timu yake katika mashindano mbalimbali yanayoendelea

Bao alilofunga nyota huyo raia wa Ivory Coast katika mchezo wa juzi dhidi ya Tabora United, limemfanya afikishe mabao nane katika mashindao yote mpaka sasa

"Nafurahia kuifungia timu yangu, nataka niwe nafanya hivi katika kila mechi ninayopata nafasi ya kucheza, malengo yangu ni kufunga angalau mabao 17 msimu huu," alisema Guede

Mshambuliaji huyo alisema ataendelea kushirikiana na wachezaji wenzake kuhakikisha Yanga inafikia malengo yake msimu huu kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kutetea Kombe la FA

"Nadhani bado tupo katika malengo yetu kama klabu na hilo ndio la muhimu, kikubwa ni kuhakikisha tunafikia malengo yetu msimu huu," alisema Guede

Kuhusu kiwango cha mshambuliaji huyo, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, alisema anafurahishwa na jitihada na uwezo wake

"Amekuwa na kiwango kizuri, anatufungia kila mechi, nafurahishwa na uwezo wake na kila anachokitoa kwa ajili ya timu," alisema Gamondi

Kocha huyo aliongeza anaamini Guede ataendelea kufanya vizuri baada ya kuwa tayari amezoa ligi ya Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’