Mapema leo, Yanga iliwasili mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Lake Tanganyika
Habari kubwa ni aina ya mapokezi ambayo Yanga imepata kutoka kwa mashabiki wake mkoani humo
Hii inaonyesha ni kiasi gani Wananchi wa Kigoma 'wali-miss' timu yao ambayo ina miaka takribani miwili haijachza mechi ya ushindani mkoani humo
Mara ya mwisho Yanga ilicheza mechi ya ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting 2021/22
Kwa mara nyingine, kesho kunako uwanja wa Lake Tanganyika Wanakigoma watapata burudani kutoka kwa mabingwa wa nchi..!










ADVERTISE HERE