Vinara wa Ligi Kuu ya NBC Yanga wako mkoani Kigoma ambapo jioni ya leo watashuka katika uwanja wa Lake Tanganyika kumenyana na Mashujaa Fc
Ni mechi ya Ligi Kuu inayokutanisha timu mbili zenye malengo tofauti. Yanga wanazihitaji alama tatu ili kuzidi kujisogeza karibu na ubingwa wakati Mashujaa wanapambana kujinusuru na janga la kuteremka daraja
Yanga ilitua Kigoma mapema jana na jioni kupata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Lake Tanganyika
Katika Mkutano na Wanahabari jana, Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi alisema wamejiandaa na mchezo huo, lengo lao ni kushinda licha ya kutambua haitakuwa rahisi mbele ya timu ngumu ya Mashujaa Fc
Kama Yanga itashinda mchezo huo itafikisha alama 65 na kuhitaji alama nyingine nane kutoka mechi tano zitakazokuwa zimebaki ili kutwaa ubingwa