Usajili mpya Yanga ni huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 May 2024
Usajili mpya Yanga ni huu

Ligi Kuu ya NBC inaelekea mwishoni ambapo May 28 jamvi la msimu huu litakunjwa rasmi na kuanza maandalizi ya msimu ujao

Yanga iko katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo ambapo wananchi wanahitaji alama nane tu ili kuhifadhi taji la Ligi Kuu kwa mara ya 30

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliweka wazi malengo ya Yanga msimu ujao ni kufanya vyema zaidi hasa katika michuano ya Kimataifa

Na hii ndio sababu Yanga itafanya maboresho kwenye nafasi zenye mapungufu katika dirisha la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao

Mpaka sasa kuna orodha ya nyota ambao huenda msimu ujao watavaa uzi wa Yanga. Hersi wakati huu yuko busy kukamilisha michakato mapema

Katika eneo la ushambuliaji linatarajiwa kuongezewa nguvu ambapo inaelezwa kuna usajili unasubiri kutangazwa tu

Prince Dube 'Mwana wa Mfalme' aliitumikia Azam Fc katika msimu huu kabla ya kuamua kuachana na timu hiyo kwa kile alichoeleza hana furaha

Dube aliwashinda Azam Fc katika madai yao ya kuwa na mkataba nae hadi mwaka 2026. Mkataba huo mpya waliodai Azam Fc haukuwa umeingizwa katika mfumo wa usajili wa TFF na FIFA ambapo taarifa za mkataba wa Dube zilionyesha mkataba wake na Azam Fc unamalizika mwishoni mwa msimu huu

Hivyo Dube akatakiwa kulipa fedha ambazo Azam Fc walithibitisha kumpatia kwa ajili ya mkataba mpya ambapo baada ya hatua hiyo kukamilika atakuwa huru

Safu ya ulinzi upande wa kushoto pia inatarajiwa kuwa na maboresho ambapo jina la mlinzi wa Fc Lupopo Chadrak Boka limetajwa

Mkataba wa Joyce Lomalisa unaelekea ukingoni na taarifa za ndani zimedokeza kuwa Yanga haitamuongeza mkataba mpya kutokana na muda mwingi kuwa nje akiwa majeruhi

Boka (24) yuko katika nyakati bora zaidi katika klabu ya FC Lupopo ambapo pamoja na Yanga pia anatajwa kuwaniwa na klabu za Tp Mazembe , Petro de Luanda na Wydad

Injinia Hersi alikuwa DR Congo wiki iliyopita, tetesi ni kuwa tayari amekamilisha usajili wa mlinzi huyo huku pia kukiwa na taarifa kuwa kuna 'surprise' kutoka pale Lubumbashi kunako klabu ya TP Mazembe

Hersi ni shabiki mkubwa wa yule winga anayevaa jezi namba 7 (Felippe Kinzumbi) na jana Yanga iliweka hadharani picha zikimuonyesha Hersi akiwa na Mmiliki wa Mazembe Mois Katumbi!. Hersi hajawahi kushindwa akiwa na jambo lake...! 

Kwa upande wa wachezaji wa ndani, kiungo mkabaji wa Singida FG Yusuph Kagoma nae inaelezwa ni suala la muda, Yanga ikiwa tayari imemsajili ili kuongeza nguvu katika eneo la kiungo kukiwa na taarifa kuwa Zawadi Mauya huenda akaondoka mwishoni mwa msimu

Lakini pia kuna ile ahadi ya bango pale kwa jirani! Anatajwa Kibu Denis. Huyu ndiye 'rastaman' ambaye amewafanya viongozi wa upande ule washikwe na butwaa baada ya kuwagomea kusaini mkataba mchana kweupeeee!

Ni wazi katika dirisha la usajili lijalo Yanga haitafanya usajili mkubwa kwani mpaka sasa Miguel Gamondi ameridhishwa na ubora wa kikosi chake kwa asilimia kubwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’