Kwa kuzingatia takwimu, kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki ana sifa zote za kuondoka na tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu huu
Ki ndio mchezaji aliyeshinda tuzo nyingi zaidi za mchezaji bora wa mwezi katika msimu huu akiwa nazo tuzo nne
Katika mbio za ufungaji bora, Ki anaendelea kuchuana na Feisal Salum wa Azam Fc wote wakiwa wamefunga mabao 15 na kutoa pasi 7 za mabao
Mechi tano za kuhitimisha msimu zitaamua nani anakwenda kuibuka mfungaji bora
Tuzo nyingi za mchezaji bora wa mwezi zinatosha kumpa Ki tuzo ya mchezaji bora wa msimu, kama haitakuwa hivyo yatakuwa maajabu mengine ya soka la Tanzania
Aziz Ki amekuwa na msimu bora katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi, akifunga na kutengeneza nafasi kwa wengine
Aidha kwa upande wa tuzo ya kocha bora wa msimu, hii pia inapaswa kuwa mikononi mwa 'Master' Gamondi yeye akiwa na tuzo tatu za kocha bora wa mwezi huku pia akikaribia kuipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu