Yanga imeendelea kusogelea ubingwa baada ya ushinda wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Mfalme wa Azam Complex, Mudathir Yahya ameendelea kuibeba Yanga mabegani akifunga bao pekee la ushindi katika dakika ya 83
Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi Kagera Sugar wakipaki basi na kutumia mbinu za kupoteza muda zaidi
Pengine Yanga ilistahili kupata ushindi mnono zaidi kwa kuzingatia nafasi walizotengeneza lakini haikuwa bahatiΒ
Aidha Joseph Guede alifunga bao kwenye dakika za majeruhi lakini lilikataliwa katika mazingira ya offside ambayo hata hivyo haikuwa sahihi
Yanga imefikisha alama 68 na sasa inahitaji alama tano tu kutwaa ubingwa
ADVERTISE HERE