Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar jana ulikuwa ushindi wa 13 kwa Yanga katika uwanja wa nyumbani msimu
Yanga haijadondosha alama katika mechi zote ilizocheza nyumbani katika ligi Wananchi wakisalia na mechi mbili nyumbani ili kuweka rekodi ya kushinda mechi zote 15 katika uwanja wa nyumbani
Aidha ushindi huo dhidi ya Kagera Sugar ulikamilisha vipigo kwa timu zote 15 zilizokutana na Yanga katika ligi msimu huu. Ni Kagera Sugar iliyokuwa bado haijaonya kichapo kutoka kwa Yanga
Wananchi sasa wameshinda jumla ya mechi 25 mfululizo nyumbani ukichukua takwimu za tangu msimu uliopita
Mpaka sasa Yanga imepachika mabao 57 huku ikiruhusu mabao 12 wananchi wakihitaji kufunga mabao manne katika mechi nne zilizosalia ili kufikia rekodi ya mabao 61 ya msimu uliopita
Kama Yanga itashinda mechi nne zilizobaki itafikisha alama 80, ambazo ni alama mbili juu ya alama 78 ambazo walikusanya msimu uliopita
Ili kukamilisha hesabu za ubingwa Yanga inahitaji alama tano tu kutoka mechi nne zilizobaki na kufikisha alama 73 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote
Lakini kama Azam Fc itapoteza au kutoka sare dhidi ya Simba Wananchi wanaweza kushangilia ubingwa mapema zaidi pengine katika mchezo unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa May 13 mkoani Morogoro