Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimethibitisha kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara wamemalizana na mshambuliaji wao wa zamani Lazarus Kambole aliyefungua kesi ya madai FIFA na kupelekea Yanga kuzuiwa kusajili
Yanga haikukamilisha kwa wakati awamu ya mwisho ya malipo ya mchezaji huyo ambapo FIFA ilitoa siku 45 kuitaka Yanga kumaliza madai hayo
Baada ya kuchelewa kukamilisha malipo ndani ya muda huo, FIFA ikawawekea Wananchi zuio la usajili
Zuio hilo sasa litaondolewa na Yanga kuwa huru kusajili wachezaji wapya
Wakati msimu ukielekea ukingoni, tayari michakato ya usajili imeanza ambapo Yanga inatarajiwa kuongeza nyota wapya pale dirisha litakapofunguliwa Julai 1
ADVERTISE HERE