Yanga inahitaji kushinda angalau mchezo mmoja kutoka mechi nne zilizobaki ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu wa tatu mfululizo
Huo utakuwa ubingwa wa 30 kwa Yanga katika historia ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amedokeza kutakuwa shamra shamra kubwa za ubingwa huo pengine kuliko wakati mwingine wowote
"Mwaka huu Yanga tunaweka rekodi ya kubeba ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya 30 inshallah.."
"Mliwahi kuona/kusikia party za ubingwa lakini jambo ambao nawahakikishia Wananchi, Party ya ubingwa mwaka huu Dunia itasema," aliandika Kamwe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Yanga inasubiri kutimiza alama za kuwa mabingwa ili kutangaza ratiba nzima ya shamrashamra hizo
Msimu uliopita Yanga ilikabidhiwa taji la Ligi Kuu mkoani Mbeya na kufuatiwa na parade kubwa la ubingwa iliyofanyika Dar es salaam siku iliyofuata
Katika msimu huu mechi mbili za mwisho zitapigwa jijini Dar es salaam hivyo kuna uwezekano mkubwa uongozi ukachagua moja ya mechi hizo kukabidhiwa ubingwa
Mchezo wa mwisho ni dhidi ya Tanzania Prisons, May 28 pengine kama mambo yatakwenda sawa, huenda mtanange huo ukapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na kufuatiwa na sherehe za kukabidhi taji kwa Mabingwa!