Wito kwa Wana Jangwani wote

Admin By Admin
β€’
12 Apr 2018
Wito kwa Wana Jangwani wote
Humu ndani sasa tuko zaidi ya elfu sabini, kwa kweli ni jambo jema limefanyika kutuunganisha idadi hiyo kubwa ya WanaYanga.

Imekuwa vizuri pia kuwa wengi wetu tumekuwa wastaarabu na tumekuwa tukilitumia vyema jukwaa letu la Mijadala.

Lengo la Jukwaa hilo ni kwa kila mwenye mawazo mazuri na kuijenga Yanga, mwenye taarifa muhimu, mwenye maswali juu ya maswala mbalimbali yanayoihusu Yanga kuuliza hapo. Majibu anayapata hapohapo.

Humu ndani wapo viongozi ambao huwa wanasoma mawazo ya WanaYanga wa humu kama ilivyo kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Mawazo mazuri yanafanyiwa kazi.

Hivyo tunawakumbusha tu, sisi huku sio kama huko kwingine, sisi huku ni kama ndugu. Matumizi ya kugha zisizofaa hayaruhusiwi.

Sisi ni washabiki tuliostaarabika. Tunakumbushana, humu tusitumie lugha za matusi, lugha za kuudhi tusiwashambulie viongozi wa Yanga kwa lugha zisizofaa.

Unaweza kujenga hoja yako ya kusifia au kukosoa vizuri tu bila kutukana.

Tufurahi pamoja timu inaposhinda lakini pia tuhuzunike pamoja timu inaposhindwa. Huo ndio ushabiki halisi.

Shabiki wa kweli ni shabiki ambaye anakuwa na timu pale inapokuwa kwenye wakati mgumu, Kwani wakati mgumu hupita tu.

Shabiki ambaye anakuwa na timu wakati inaposhinda na kuiona haifai inapokuwa haifanyi vizuri huyo ni MAMLUKI.

Hivyo tukifungwa tuwe wavumilivu, tukishinda tufurahi. Tunapokuwa hatufanyi vizuri tuwasaidie viongozi wetu kwa kutoa maoni ya kujenga.

MBARIKIWE SANA

MUHIMU
Kwa wale ambao hawaja Update App zao, kuna toleo jipya tayari liko Play Store. Kuna maboresho zaidi yamefanyika kuiboresha App yetu. Tembelea Play Store ku Update.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’