Hivi karibuni, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki (CECAFA) lilitangaza kurejea michuano ya CECAFA Kagame Cup itakayoshirikisha timu 16
Michuano hiyo inarejea baada ya kusimama kwa miaka miwili tangu 2021 ilipofanyika mara ya mwisho jijini Dar es Salaam
Tanzania imepewa wenyeji wa michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi Agosti 4 2024
Kati ya washiriki 16, timu 12 zimetoka katika jumuiya wanachama, ikiwamo Zanzibar, na timu nyingine nne zilizoalikwa
Mara ya mwisho michuano hiyo ilipofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania, mwaka wa 2021, Express FC ya Uganda iliifunga Nyasa Big Bullets ya Malawi bao 1-0 kwenye fainali
Vyama wanachama wa CECAFA ni pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Sudan Kusini, Sudan, Ethiopia, Eritrea, Zanzibar, Somalia, Rwanda, Burundi, na Djibouti
Yanga ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC hivyo moja kwa moja wataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano hiyo
Hata hivyo ratiba inaweza kuathiri Tamasha la wiki ya Mwananchi ambapo kuna uwezekano mkubwa Tamasha hilo likafanyika mapema kabla ya michuano ya KAGAME CUP kuanza
Michuano hii itakuwa sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya hasa mechi za hatua ya awali Ligi ya Mabingwa ambazo zitafanyika mwanzoni mwa August