Mechi dhidi ya Ihefu Fc itakuwa ngumu - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2024
Mechi dhidi ya Ihefu Fc itakuwa ngumu - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anatambua mchezo wa nusu fainall kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha utakuwa mgumu

Hata hivyo Gamondi amesema ana imani na ubora wa kikosi chake malengo ya yakiwa ni kushinda mchezo huo na kutinga fainali

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi amesema wamepata muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo baada ya mechi ya mwisho ya ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar iliyowahakikishia kutwaa ubingwa

"Tumekuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchezo huu, tumepata muda mzuri wa maandalizi baada ya mechi yetu ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar"

"Mchezo wa kesho ni mchezo mkubwa na hautakuwa mchezo rahisi lakini sisi ni washindani na tutahakikisha tunapambana kupata ushindi na kwenda fainali"

"Tunaamini tuna kila sababu ya kuendelea kufanya vizuri msimu huu, tuna Wachezaji wanaopenda kutafuta magoli na kufunga ndio maana wachezaji wetu wapo kwenye orodha ya wafungaji bora kwenye kila mashindano," alisema Gamondi

Yanga ilitua Arusha jana na leo watapata muda wa kufanya mazoezi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao mchezo huo utapigwa Jumapili, saa 9:30 Alasiri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’