Baada ya kutua Dar usiku kutoka Arusha, Yanga haina muda wa kupoteza kwani imeelekea mkoani Dodoma tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji
Mchezo huo utapigwa kesho Jumatano, May 22 katika uwanja wa Jamhuri
Jumatano ni Gamond Day, mechi maalum ya kumpa heshima Kocha Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi baada ya kazi nzuri waliyoifanyia Yanga msimu huu
Baada ya kuumana na Dodoma Jiji hapo kesho, mapema siku ya Alhamisi, Yanga itakuwa bungeni kuhudhuria mwaliko wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas NdumbaroΒ
Jioni ya siku hiyo kikos kitarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu zitakazofanyika Jumamosi, May 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya mchezo dhidi ya Tabora United
Burudani inahamia Makao Makuu DODOMA@AirTanzania#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/EP78plBuSK
β Young Africans SC (@YoungAfricansSC) May 21, 2024