Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema sasa ni muda wa kuvunja rekodi zote msimu huu
Baada ya kuisaidia Yanga kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo pamoja na kutinga fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB, macho ya Aziz Ki sasa yako kwenye tuzo ya ufungaji bora
Jana Feisal Salum alifunga bao la 16 na kumfanya akae kileleni katika vita ya ufungaji bora akimuacha Aziz Ki na mabao yake 15
Kama Aziz Ki atafunga dhidi ya Dodoma Jiji leo basi atarejesha matumaini yake ya kushinda tuzo hiyo ambayo msimu uliopita Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza waligawana baada ya kufunga mabao 17 kila mmoja
Yanga itahitimisha mechi mbili za mwisho jijini Dar es salaam dhidi ya Tabora United na Prisons
Mechi ya Tabora United itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi, siku ambayo Yanga itakabidhiwa ubingwa