Habari kubwa leo ni paredi la ubingwa wa 30 wa Yanga lililoanza uwanja wa Benjamin Mkapa na kuhitimishwa Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani
Wananchi walijitokeza kwa wingi wakianza na kunywa supu pale kwa Mkapa kabla ya kuanza paredi liliofunga kabisa mitaa ya Kariakoo kwa takribani masaa mawili
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alipata nafasi ya kutoa salamu za shukrani kwa Wananchi ambapo pamoja na mambo mengine, aliwahakikishia furaha itaendelea kutawala Jangwani
"Nawashukuru wote mliojitokeza hapa, niwahakikishie timu yenu itaendelea kuwa imara, hatutapoteza mchezaji yeyote katika dirisha la usajili. Tutafanya usajili wa wachezaji bora zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya klabu yetu"
"Msimu huu tulifanikiwa kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa, malengo yetu msimu ujao ni kufika mbali zaidi"
"Bado hatujamaliza msimu, tunaomba muendelee kutuunga mkono, tunawaahidi tarehe 2 Juni tunakwenda kucheza fainali nyingine na tutaleta kombe hapa kusherehekea kwa mara nyingine," alisema Hersi