Kesho Jumanne, May 28 2024 Yanga itahitimisha msimu wa ligi kuu 2023/24 kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex, saa 10 jioni
Yanga imetangaza viingilio vya mechi hiyo ya mwisho msimu ambapo VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B Tsh 10,000/- na Mzunguuko Tsh 5,000/-
Tayari ubingwa uko Jangwani iliyobaki ni kuhakikisha tuzo ya mfungaji bora nayo inatoka Jangwani
Ni mechi ya kumsimika Stephane Aziz Ki kuwa mfungaji bora wa ligi kuu msimu huu
ADVERTISE HERE