Yanga inatajwa kumalizana na mlinzi wa kushoto kutoka klabu ya Fc Saint Eloi Lupopo Chadrack Issaka Boka raia wa DR Congo
Boka anatarajiwa kuchukua nafasi ya Joyce Lomalisa aliyeomba kuondoka baada ya mkataba wake kumalizika
Wakala wa Boka alikuwa nchini kukamilisha mchakato wa usajili huo makubaliano yakiwa ni miaka miwili
Kwa takribani miezi kadhaa Yanga ilikuwa ikumuwinda beki huyo anayesifika kuwa na kasi na uwezo wa 'kumwaga maji' kama ilivyokuwa kwa Lomalisa
Wakati alipokuwa DR Congo Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alipata nafasi ya kumshuhudia katika moja ya mechi za Fc Saint Eloi Lupopo
ADVERTISE HERE