Tutawaheshimu Azam Fc - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jun 2024
Tutawaheshimu Azam Fc - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa New Amaan Complex

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi alisema wamekuwa na muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo hivyo wako tayari

Aidha Gamondi amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na tahadhari kubwa kwani wanatambua ubora wa Azam Fc

"Tumepata muda mzuri wa maandalizi na leo tutafanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wetu wa fainali kesho"

"Niwapongeze kwa kuchagua Uwanja wa Zanzibar kwa sababu ni uwanja mzuri wa kisasa na watu wa Zanzibar pia wataweza kupata nafasi ya kushuhudia fainali hii kubwa"

"Kwenye mpira hakuna kulipiza kisasi ukienda kwenye mchezo kwa nia ya kulipiza kisasi hutakuwa na mchezo mzuri, namuheshimu mpinzani wangu Azam na lazima twende tukacheze mchezo wenye mbinu nzuri ili tuweze kuibuka na ushindi"

"Yanga na Azam Fc wamekuwa na michezo bora msimu huu, najua kesho kutakuwa na upinzani mkubwa na sisi tumejiandaa na hilo," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’