Taji la FA linarudi kwa Wananchi kwa ushindi wa mikwaju ya penati 6-5 dhidi ya Azam Fc baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Ulikuwa mchezo mgumu ambao hata hivyo Yanga walitengeneza nafasi zaidi lakini hawakuzitumia vyema huku pia mlinda lango wa Azam Fc akiwa kikwazo
Wanasema mikwaju ya penati haina mwenyewe hicho ndicho kilichotokea kwani Yanga ilipoteza penati mbili za awali lakini ikafanikiwa kubaki mchezoni kwa kufunga peneti tatu zilizofuata huku Azam Fc wakikosa penati mbili za mwisho
Ni kombe la pili kwa Yanga msimu huu likiwa taji la FA kwa msimu wa tatu mfululizo
Beki Ibrahim Bacca alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo huku Clement Mzize akiibuka mfungaji bora na mabao yake matano

Hongera Wananchiiiiiiiiiiiii
ADVERTISE HERE