Yanga kuanzia raundi ya pili Ligi ya Mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jun 2024
Yanga kuanzia raundi ya pili Ligi ya Mabingwa

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga hawatacheza hatua ya awali ya mashindano ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakayoshiriki katika msimu mpya wa michuano hiyo

Yanga ni miongoni mwa timu mbazo zimekidhi vigezo vya kuanzia raundi ya pili ya michuano hiyo kama ilivyo kwa watani zao Simba ambao hata hivyo wako kombe la Shirikisho

Timu nyingine za Tanzania Bara zitakazoshiriki mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) msimu ujao, ni Azam FC ambayo itapambana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Coastal Union kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika

Hata hivyo, Azam na Coastal Union, zenyewe zitaanza michuano hiyo kwenye hatua ya awali na mechi zao za kwanza zitachezwa nyumbani kati ya Agosti 16 na 18, mwaka huu

Katika taarifa iliyotolewa na CAF, inasema klabu hizo mbili kutoka Tanzania, Yanga na Simba zitaanza kuwania ubingwa wa mashindano kuanzia raundi ya pili na mechi zao za kwanza zitachezwa ugenini na kumalizia nyumbani

CAF katika taarifa yake imesema pia hatua ya awali ya mashindano hayo ya ngazi ya klabu kwa msimu wa 2024/2025 itaanza rasmi kufanyika kati ya Agosti 16 na 18, mwaka huu

Shirikisho hilo pia limesema mechi za hatua ya makundi zitafanyika kati ya Oktoba na Desemba, mwaka huu huku michezo ya mtoano ya mashindano yote ikitarajiwa kuchezwa kati ya Machi na Mei, mwakani

CAF pia imethibitisha nchi 12 ambazo zina pointi nyingi katika viwango vya ubora vitatoa timu mbili katika kila mashindano (mbili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na mbili katika Kombe la Shirikisho Afrika), ni pamoja na Algeria, Angola, Ivory Coast, Misri, Libya, Morocco, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Afrika Kusini, Sudan, Tunisia na Tanzania

Wakati huo huo CAF pia imefungua ukurasa kwa nchi wanachama wake kuwasilisha majina ya timu zitakazoshiriki mashindano hayo Mfumo wa Mashindano wa shirikisho hilo (CMS)

Timu zitakazoshiriki mashindano hayo pia zitatakiwa kufuata kalenda ya usajili ambayo itaanza Julai Mosi hadi 20, mwaka huu kwa ajili ya wachezaji watakaocheza mechi za hatua ya awali wakati usajili utakaoanza Julai 21 hadi Agosti 31 utawahusu nyota watakaoshiriki mechi ya hatua ya pili

Dirisha lingine la tatu litafunguliwa kuanzia Septemba Mosi hadi 30 na litawahusu wachezaji watakaoshiriki mechi za hatua ya makundi na timu zitakazosonga mbele katika michuano hiyo zitaruhusiwa kuongeza idadi ya wachezaji wasiozidi saba katika kipindi cha Januari Mosi hadi 31, mwakani

Iliongeza hatua ya pili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho imeondolewa wakati timu zitakazotolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika hazitahamia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kama ilivyokuwa misimu iliyopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’