Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida United, mchezo wa ligi unaofuata ni dhidi ya Simba April 29 2018.
Kwa sasa Yanga imeelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha unaopigwa Jumatano ijayo.
Kwa hakika mchezo huo wa watani wa jadi ndio utaamua hatma ya ubingwa kwa kikosi cha Yanga msimu huu.
Yanga ni lazima ishinde, matokeo yoyote tofauti na ushindi yataiondoa kabisa kwenye mbio za ubingwa.
Awamu hii Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa imeimarika zaidi tofauti na mchezo wa kwanza.
Mchezo wa kwanza uliopigwa mwaka jana Oktoba 28 kwenye uwanja wa Taifa ulizishuhudia timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1.
Juzi nahodha wa Yanga Nadir Haroub baada ya mchezo dhidi ya Singida United aliwaambia waandishi wa habari kuwa watahakikisha wanashinda mchezo huo wa April 29.
Jambo la msingi kwa wapenzi na wanachama wa Yanga ni kutomruhusu 'bundi' anayezengea klabuni kuwavuruga katika kipindi hiki muhimu sana.
Njia pekee ya kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo na michezo mingine iliyobaki ni umoja na mshikamano.

ADVERTISE HERE