Ilikuwa misimu miwili ya kibabe kwa Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Jun 2024
Ilikuwa misimu miwili ya kibabe kwa Aziz Ki

Ilikuwa misimu miwili ya kibabe kwa Stephane Aziz Ki ambaye msimu huu ameibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC baada ya kufunga mabao 21 huku akitoa assist nane

Takwimu zake zimemuweka katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP) kama yale mambo ya 'kubalance' hayatafanyika. Tumeona kilichotokea kwenye tuzo ya mchezaji bora na kocha bora wa ligi kuu kwa mwezi May 2024!

Katika msimu wake wa kwanza na Yanga, Aziz Ki alifunga mabao 9 na kutoa pasi tatu za mabao na hivyo katika misimu yote miwili amefunga mabao 30 na kutoa assist 11 akihusika katika mabao 41 yaliyofungwa na Yanga

Katika misimu ya karibuni Fiston Mayele na Aziz Ki ndio wachezaji waliohusika katika mabao mengi zaidi yaliyofungwa na Yanga

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewahakikishia Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuwa wataendelea kumshuhudia Aziz Ki msimu ujao

Kinachosubiriwa ni taarifa za nyota huyo kusaini mkataba mpya kama ilivyo kwa wachezaji wengine waliomaliza mikataba

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wataanza kuachia taarifa za wachezaji wanaoondoka na wale walioongeza mikataba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’