Yanga haina mpango wa kuachana na mlinda lango Aboutwalib Mshery licha ya tetesi zinazodai mlinda lango huyo ameomba kuondoka sababu ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza
Mshery ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao imemalizika, hata hivyo tayari Yanga imekamilisha nae mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya
Yanga inamtazama Mshery kama mrithi sahihi wa Djigui Diarra ambaye kwa misimu mitatu amekuwa tegemeo katika kikosi cha Yanga
Msimu uliopita Mshery aliaminiwa katika baadhi ya mechi na alionyesha ameiva na yuko tayari kwa majukumu makubwa
Yanga imemuhakikishia Mshery kuwa bado anahitajika na atapata nafasi zaidi ya kucheza kuanzia msimu ujao
Baada ya kuachana na Metacha Mnata, Yanga pia inatarajiwa kusajili mlinda lango mwingine wa ndani