Kiungo mshambuliaji wa Yanga Farid Mussa ataendelea kuwatumikia Wananchi baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili
Mkataba wake wa awali na Yanga umemalizika lakini nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Miguel Gamondi amewahitaji katika kikosi chake
Farid anayemudu kucheza kama kiungo mshambauliaji, winga na beki wa kushoto, alijiunga na Yanga Agosti, 2020 akitokea Tenerife ya Hispania
Nyota huyo wa zamani wa Azam, alikuwa akihusishwa kurejea kwa waajiri wake hao wa zamani
Tangu aliporejea Tanzania kutoka Hispnia na moja kwa moja kujiunga na Yanga, Farid ameshinda mataji nane pia akiwa na medali ya fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC)
ADVERTISE HERE