Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo iko ugenini nchini Zambia kuwakabili majirani zao hao katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Dunia 2026
Itakuwa mechi ya raundi ya tatu kwa Stars wakati Zambia ikiwa mechi ya nne katika kundi E
Zambia walipoteza mechi yao iliyopita dhidi ya Morocco kwa kufungwa mabao 2-1 wakati mechi ya Tanzania dhidi ya Elitrea ilifutwa baada ya timu hiyo kujiondoa mashindanoni
Morocco ndio vinara wa kundi E wakiwa na alama sita baada ya kushinda mechi zao zote mbili wakati Zambia, Niger na Tanzania zote zina alama tatu zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa (GD)
Mchezo unatarajiwa kupigwa uwanja wa Levy Mwanawasa kuanzia saa 1 usiku na Azam Media wataonyesha mbashara
ADVERTISE HERE