Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam leo kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha.
Yanga imeondoka na kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 13, nane wakiwa wa benchi la Ufundi.
Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib hayumo kwenye msafara huo. Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema Ajib ni majeruhi.
Andrew Vicent Chikupe naye ameshindwa kupona kwa wakati majeraha aliyopata kwenye mchezo uliopita, hakusafiri.
Wengine ambao hawajasafiri na timu ni pamoja na Donald Ngoma, Amissi Tambwe (majeruhi), Said Mussa, Ramadhani Kwabwili (majukumu ya timu ya Taifa), Maka Edward na Baruani Akilimali.
WACHEZAJI WALIOSAFIRI
Makipa : Youthe Rostand, Benno Kakolanya.
Mabeki : Hassan Kessy, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Kelvin Yondani na Nadir Haroub.
Viungo : Raphael Daudi, Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Said Juma, Thaban kamusoko, Yusuph Mhilu, Geofrey Mwashiuya na Emmanuel Martin
Washambuliaji : Obrey Chirwa, Juma Mahadhi na Yohana Mkomola.

ADVERTISE HERE