Kocha na mtaalam wa tiba ya viungo, Mtunisia Youssef Ammar amemaliza mkataba wa kuitumikia Yanga
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa Yanga italeta mtaalam mwingine wa viungo kwa kuzingatia mapendekezo ya Kocha Miguel Gamondi
Ammar amethibitisha kumalizana na Yanga huku akelezea kufurahia mafanikio na maisha mazuri aliyoishi ndani ya Yanga
"Nilikuwa na misimu mitatu bora kutokana na mafanikio ya timu lakini najivunia kufanya kazi kwa ubora katika kipindi chote nilichokuwa hapa," alisema Ammar
Ammar aliletwa na kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi ambapo alichagua kubaki Yanga pale Nabi alipoondoka msimu uliopita
Akiwa na Yanga, Ammar ametwaa mataji mbalimbali, Ligi Kuu Bara (3) na mawili Kombe la Shirikisho (FA), huku akiwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo ilipocheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2022/23 na msimu uliomalizika wacheza hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika