Winga Skudu Makudubela yawezekana asiwe sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao kwani nyota huyo hayupo katika mipango ya kocha Miguel Gamondi
Uongozi wa Yanga uko katika mchakato wa kuachana na winga huyo aliyepachikwa jina la Waziri wa raha
Skudu alisaini mkataba wa miaka miwili wakati anatua Yanga hivyo njia ya kuachana nae ni kuvunja mkataba au kumtoa kwa mkopo katika moja ya klabu huko Afrika Kusini
Mpaka sasa tayari Yanga imemalizana na Augustine Okrah ambaye makubaliano ya kuvunja mkataba wake yalifikiwa
Aidha kulikuwa na mpango wa kumtoa Kennedy Musonda kwa TP Mazembe lakini jambo hili ni kama halitawezekana baada ya Mazembe kumuuza Fellipe Kinzumbi kwenda Raja Athletic
Yanga ilitaka kumtumia Musonda kumnasa Kinzumbi katika makubaliano ya kubadilishana wachezaji
Lakini Mazembe wakahitaji wapewe Musonda na fedha ili wamtoe Kinzumbi jambo ambalo uongozi wa Yanga haukukubaliana nalo
Kuna taarifa kuwa Mazembe wamewasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili Musonda, ofa ambayo huenda Yanga wasiikubali
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema watafanya 'usajili wa kutisha' kwa kuzingatia malengo ya msimu ujao ambayo ni kutetea mataji yote ya ndani ya angalau kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa