Wape Tabasamu ni leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2024
Wape Tabasamu ni leo

Mkoa wa Morogoro siku ya leo Jumamos utapata ugeni mkubwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ambapo Wananchi watafurika kushuhudia Tamasha la Wape Tabasamu lililoandaliwa na nyota wa Yanga Kibwana Shomari na Dickson Job

Ni mechi ya 'charity' kwa ajili ya kuchangisha fedha ambazo zitakwenda kusaidia wale wenye uhitaji

Ni msimu wa tatu Job na Kibwana wanaandaa Tamasha hili lakini mwaka huu linaonekana kuwa na mvuto zaidi

Ushindani ni mkali kuanzia katika usajili wa wachezaji lakini hata 'mabosi' nao kuchagua upande

GSM pamoja na Arafat Haji wao wamechagua upande wa Kibwana wakati Injinia Hersi Said yeye yuko upande wa Job

Wachezaji kama Pacome Zouzoua, Clatous Chama, Prince Dube wanatarajiwa kuitumikia timu Job wakati vinara wa mabao ligi kuu msimu uliopita Stephane Aziz Ki aliyekuwa mfungaji bora na Feisal Salum aliyeshika nafasi ya pili wako timu Kibwana bila kumsahau Mukoko Tonombe

Kumekuwa na matukio ya 'kuporana' wachezaji ambapo beki Ibrahim Bacca ambaye awali alitangaza kuwa timu Kibwana jana alionekana akisaini kuitumikia timu Job kwa kile alichoeleza timu Kibwana hawana hela!

Ni katika 'kunogesha' Tamasha hilo ambalo mafanikio yake yatapeleka Tabasamu kwa watu wengi zaidi

Treni ya mwendokasi kutoka jijini Dar es salaam imepeleka mashabiki mkoani Morogoro na kuwarudisha Dar baada ya mchezo jioni ya leo

Azam TV nao watakuwa mbashara Baraka Mpenja akipewa jukumu la kuhabarisha yatakayojiri dimba la Jamhuri kuanzia saa 10 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’