Kalenda ya mashindano ya CAF msimu wa 2024/25 inaanza mapema ambapo mechi za hatua ya awali zinatarajiwa kupigwa mwanzoni mwa August 2024
Kulingana na kalenda iliyotolewa mwanzoni mwa mwezi huu, droo ya mechi za hatua ya awali itafanyika Julai 04 huko Misri wakati mechi za awali mkondo wa kwanza zitapigwa August 16-18
Habari njema kwa Yanga ni kuwa huenda isicheze hatua ya awali ikiwa miongoni mwa timu 10 bora katika 'ranking' ya CAF ya miaka 5
Yanga inashika nafasi ya 8 katika 'ranking' miongoni mwa timu zinazoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa 2024/25
Al Ahly, Esperance, Mamelodi, Petro Atletico, TP Mazembe, CR Belouizdad na Raja Casablanca ndio timu zilizo juu ya Yanga
Kama Yanga itafanikiwa kutinga hatua ya makundi, katika droo ya hatua hiyo itaweka poti namba 2 pamoja na TP Mazembe, CR Belouizdad na Raja
Msimu uliopita Yanga iliwekwa poti namba 3 na kuangukia kundi D ikiwa na Al Ahly, CR Belouizdad na Medeama