Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliopita, kikosi cha Yanga U17 kinaendelea kugawa dozi ligi ya vijana leo kikiifumua KMC mabao 5-1
Kipigo hicho kinafanana na kipigo ambacho Yanga waliwapa KMC katika mchezo wa ligi kuu msimu uliopita
Unaweza kusema 'DNA' ya timu ya wakubwa imeanza kusambaa hata kwa timu ya vijana
Wakati timu hiyo inayonolewa na kocha Vicent Barnabas ikiendelea kufanya vizuri, Yanga tayari imewaleta CSKA Moscow ambao watashirikiana nao katika program maalum ya kusaka vipaji katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga na Zanzibar
Vijana watakaopatikana katika mpango huo, wataingia katika 'project' maalum ya Yanga na wengine kupata nafasi ya kujiunga na akademy ya CSKA huko Urusi
Yanga na CSKA Moscow ziliingia makubaliano ya ushirikiano katika kutengeneza mahusiano ya kukuza vipaji kwa soka la vijana na kubadilishana taaluma mbalimbali za kimichezo na utawala