Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamealikwa nchini Rwanda kucheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa nchi hiyo APR
Taarifa kutoka Rwanda imebainisha kuwa Wananchi wa Taifa hilo wana shauku kubwa ya kuishuhudia Yanga kwa mara nyingine baada ya msimu uliopita kuliteka jiji la Kigari pale walipokwenda kucheza dhidi ya Al Merrikh katika mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika
Rais wa APR FC, Kanali Richard Karasira amethibitisha kuwa tayari wameitumia mwaliko Yanga na matarajio yao ni kuwa Wananchi watakubali
Yanga ina uhusiano mzuri na Rwanda kwani hata Rais wa nchi hiyo Paul Kagame amejipambanua kuwa shabiki mkubwa wa Yanga
Huo utakuwa mwaliko wa nne kwa Yanga ambayo kwa hakika unaweza kusema kwa sasa ni keki ya moto kutokana na mafanikio yao katika misimu mitatu iliyopita na aina ya soka lao la kupendeza
Mkononi Yanga ina mialiko ya kwenda kufanya pre-season Ulaya, kushiriki michuano maalum iliyoandaliwa na Kaize Chiefs uko Afrika Kusini na mwaliko kutoka Serikali ya Kenya kushiriki halfa ya uzinduzi wa uwanja huko Kisumu