Uongozi wa Yanga uko katika mazungumzo na mlinda lango Djigui Diarra kwa ajili ya kumuongeza mkataba
Diarra amekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya Yanga katika misimu yote mitatu ambayo Yanga imetwaa mataji ya ndani ya kufanya vyema katika mashindano ya CAF
Bado mlinda lango huyo namba moja wa timu ya Taifa ya Mali ana mkataba wa mwaka mmoja lakini Yanga inataka kumuongezea mkataba ili kupunguza presha juu ya hatma ya kipa huyo hasa pale mkataba wake utakapomalizika msimu ujao
Ni wazi pia thamani ya Diarra imepanda mara dufu kutokana na kile alichofanya katika msimu uliopita katika klabu ya Yanga na hata timu ya Taifa ya Mali
Ni kawaida klabu kufanya tathmini na kumuongezea mchezaji mshahara na marupurupu mengine pale anapofanya vizuri
ADVERTISE HERE