Baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza cha Yanga watashiriki mechi maalum ya kirafiki Jumamosi Juni 29 katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1 usiku dhidi ya Safari Champions
Mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliopita Stephane Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuhusika katika mchezo huo
Wachezaji wote wa Yanga walipewa likizo na wanatarajiwa kuanza kurejea mwishoni mwa wiki hii tayari kwa maandalizi ya pre-season
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wameuchukulia kwa uzito mkubwa mchezo huo huku akiwatahadharisha vijana wa Safari kuwa wajiandae na kipigo kizito
Yanga ina uhakika wa kuwatumia nyota wake wa ndani katika mchezo huo na baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao watarejea mapema
Viingilio vya mchezo huo;

