Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC kwa misimu mitatu mfululizo
Mwamnyeto ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao ilikuwa imemalizika
Baada ya mazungumzo ya wiki kadhaa hatimaye nyota huyo wa zamani wa Coastal Union ameongeza mkataba
Mwamnyeto amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa misimu minne akiishuhudia Yanga ikishinda mataji matatu ya ligi kuu, mataji matatu ya kombe la Shirikisho, Ngao mbili za Jamii, fainali ya kombe la Shirikisho la CAF na robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika
ADVERTISE HERE